Hekima ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu, matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya.
Katika dini mbalimbali inatokana na imani kwa Mungu.
Katika Ukristo inatajwa pengine kati ya vipaji vya roho mtakatifu vinavyokamilisha maadili ya kiutu na maadili ya kimungu vilevile (http://sw.wikipedia.org/wiki/Hekima).
Kwa ujumla, hekima ni uadilifu mzuri alionao mtu.
Katika kufanya maamuzi katika maisha yetu, hekima ndo ngao madhubuti ya kukuepusha kufanya maamuzi yasiyo sahihi kwa sababu binadamu walio wengi hufanya maamuzi yasiyo sahihi ambayo baadaye huleta madhara kwao na kwa jamii husika inayowazunguka kwa sababu ya kukosa hekima nafsini mwao.
Unapotaka kufanya maamuzi yoyote tumia hekima, kwa sababu hekima hujikita katika kutoa ukweli na uhalisia wa mambo, vilevile hekima hujitenga mbali na uongo vitu ambavyo ni vikwazo vikuu vya kufanya maamuzi kwa maana unapokua na hekima mala zoote utaegemea kwenye ukweli na uhalisia wa mambo yanayokuzunguka.
Kiongozi yoyote anahitaji hekima kwani wao ndo wanahusika katika kufanya maamuzi ya mwisho ya kundi ambalo analiongoza, kwa hiyo mtu yoyote anayekosa hekima hafai kuwa kiongozi kwa maana atakuwa anafanya maamuzi yasiyo sahihi ambayo hupotosha kundi ambalo analiongoza.
TUNAHITAJI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI KWA AJILI YA MAENDELEO, KILA MMOJA WETU ANAHITAJI KUFANYA MAAMUZI SAHIHI.
ANZA SASA FANYA MAAMUZI SAHIHI.
Asante sana kwa kusoma nakala hii.
Awadhi Changa.
Geographer & Environmentalist.
awadhchang@outlook.com
0752-393944.
No comments:
Post a Comment