Friday, August 29, 2014

MTAZAMO CHANYA HUMJENGA MTU KI-FIKRA.

Kuna baadhi ya binadamu ambao huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mawazo na maneno yenye mitazamo hasi ambayo huyapata kutoka kwa wengine, Hii pia ni kawaida tu hasa kwa binadamu yoyote ambaye ambaye ameshapitia misukosuko mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Watu wa namna hii wanahitaji sana mitizamo chanya ambayo Itawajenga ki-fikra,
Kwa sababu wakikumbuka walikotoka na maneno hasi uliyowapa kwaida hujikuta wakiwa wanyonge na walio kata tamaa, Tafadhari fikiri chanya, Ongea mitazamo chanya itakusaidia wewe pamoja na yule unayemueleza. kwa sababu unapoongea mitizamo chanya mala kwa mala, mitizamo hiyo chanya hujiweka katika ufahamu wako na kujikuta unafanya mambo mazuri ya maendeleo.
Ni vizuri sana kufanya, kuongea na kufikiri mitazamo chanya japokua mtazamo chanya hauwezi kujidhihirisha pasipokuwepo na mtizamo hasi kwa maana ili mtizamo chanya ujidhihilishe ni lazima kuwepo na mtizamo hasi kwa hiyo tufanye mitizamo chanya bila kusahau  kuwepo kwa mitazamo hasi ambayo pia ni vizuri kuitambua kusudi kuiepuka na kuikataa ili isikurudishe nyuma kwa maana ya kwamba tuitizame mitazamo hasi pia kwa kuitafutia sululisho la ukweli na uhakika kwa sababu "mtizamo chanya huwezi kuwepo pasipo mtizamo hasi kuwepo". Kwani majukumu ni kuyakabili kwanza.
Na mwisho kabisa kuna mtazamo ambao humuweka mtu katikati "neutral" ambao ni mtazamo ambao mda mwingi haufungamani na upande wowote ule, ambao mala nyingi husaidia kujiepusha na mazara ya kuegamia au kupendelea upande mmoja ambao mala nyingi hutumiwa na viongozi katika kutatua mijadala na mizozo ya makundi mbalimbali ambapo ni VIONGOZI huutumia ili kuleta suruhu. Vilevile ni vizuri kuwatoa watu wenye mitizamo Hasi na kuwapeleka kwenye kundi la watu wenye mitizamo chanya ambao unawajenga, Mbinu Hii  hutumiwa KUSULULISHA MIGOGORO NA MIZOZO MIKUBWA, mfano mzuri wa kiongozi makini ambaye hutumia mbinu hii nzuri ya kutatua Migogoro ni MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ambaye ni Raisi pekee wa Tanzania ambaye anaweza kutatua mizozo ya kisiasa yenye mivutano ya pande mbili, mfano katika hotuba yake ya ufunguzi wa BUNGE LA KUUNDA KATIBA MPYA alijitahidi kuwa kwenye mitizamo ya makundi yote na kutoa faida na hasara za Mitizamo ya makundi hayo na mwisho kabisa akajitahidi kuwavuta wale wenye mitizamo hasi ili wawe kwenye kundi la mtazamo chanya ili wawe wamoja au kitu kimoja na Hii ndo SIFA PEKEE YA MH RAISI J.K aliyonayo ambayo pia ilimfanya awe raisi bora wa Afrika na kupata tuzo ya utawala bora Afrika kwa sababu alishawahi kuwaweka pamoja makundi mawili yaliyokua  yanavutana KENYA ambapo tofauti zao zilisababisha kutokea kwa machafuko nchini mwao. KWA KWELI RAISI J.K ANASTAHILI PONGEZI MAALUM KWANI NI RAISI PEKEE WA TANZANIA ANAYEKUZA DEMOKRASIA, UELEWA (Elimu) NA UHURU, UKWELI KWA WANANCHI.
Mtizamo huu ni mzuri lakini ni vizuri kujitahidi kuegemea kwenye mtizamo chanya kwa sababu hauna madhara malanyingi HUMJENGA MTU NA KUMUEPUSHA NA MISUKOSUKO.
Mtazamo Chanya humjenga mtu kwa sababu mambo unayoyafikiri siku zote ndo zao kuu la maisha yako ya baadae kwa hiyo kama Unamtazamo chanya kwa kufikiria na kufanya mambo yako baasi jihesabie ya kwamba ni mtu mwenye maisha mazuri siku za usoni au za hapo baadaye, vile vile mambo yote unayoyafikilia huwa ndo muelekeo wako wa baadaye "IF YOU THINK SMALL YOU WILL BE SMALL ON YOUR LIFE".  
Hebu angalia mfano huu mdogo wa A Lincolin ambaye kimtazamo alitaka kurudishwa nyuma lakini hakukubaliana na hari kama hiyo kwa hiyo USIKUBALI KURUDISHWA NYUMA KWA MANENO MATUPU TU, Kwani wengine hujiona WAMESHINDWA kwa sababu ya maneno hasi ya watu, na kujikuta Wanafikiria kushindwa, ambapo fikra hizo hujengeka nafsini / akilini mwao na kujikuta wameshindwa kwa sababu fikra hizo zimejengeka akilini na nafsini mwao. SI VIBAYA KAMA UTAKUA UNAFIKIRI MITIZAMO CHANYA KWA SABABU ITAKUJENGA. Lakini si vibaya sana kama utajifunza kuitetea mitazamo yako CHANYA popote pale na kwa mtu yoyote. kwa maana mitizamo chanya huanza kujidhihirisha kutoka kwenye fikra hadi kwenye utekelezaji na utendaji wako.



"ALWAYS THINK POSITIVE TO RECEIVE POSITIVITY"
"UNAPOTEMBEA ANGALIA MBELE USITEMBEE UKIANGALIA NYUMA UTAANGUKA" 
Thanks
Awadhi Chang'a
Geographer & Enviromentalist


No comments:

Post a Comment