Wednesday, September 10, 2014

KAULI ILIYOSAHIHI INATOKA WAPI?, JIFUNZE KUONGEA MAMBO SAHIHI


FIRST DRAFT.
Maamuzi yoyote kabla ya kufikiwa ni lazima kuna kauli mbalimbali zinatolewa ili kufikia lengo mahususi,     
Kutoa kauli ni jambo kubwa sana ambalo linahitaji umakini mkubwa sana, kwani maneno yako yanaweza kuleta mabadiliko kwako na kwa mtu ambaye unamueleza, Kwa hiyo kutoa kauli sahihi au kuongea maneno sahihi kwa wakati sahihi husaidia sana kuleta mabadiliko. kwa hiyo unatakiwa kuwa makini sana unapo ongea mambo mbalimbali.
Unapo ongea kuna vitu lazima utambue kuna mambo yakuzingatia, moja ya mambo hayo ni kuzingatia kama mada hiyo ni ya wazi au si ya wazi (public or not). 

Faida ya kuongea mambo ambayo ni sahihi husaidia mtu kuwa huru na kulinda utu na heshima na kukuza status yako.

Inatakiwa kuvi expose vitu ulivyonavyo ili watu wajue vitu ulivyonavyo japokua ni lazima ujue kutenga vitu ambavyo ni hidden na vitu vya wazi. 

Pia unapotoa taarifa yoyote jitahidi kutoa taarifa ambayo ni sahihi na kuepuka kauli ambazo si sahihi kwa sababu UKWELI DAIMA HUMUWEKA MTU HURU.

Epuka kutoa taarifa ambazo hazijathibitishwa, Watu wengi hupenda kutoa taarifa ambazo wamesikia kwa watu wengine jambo ambalo si sahihi. Kimsingi unaweza ukathibitisha kauli ambazo si sahihi na kujikuta unapotosha na kujenga taswira mbaya.

Asante Sana.
Awadhi Chang'a.
Geographer -Environmentalist.

Tuesday, September 9, 2014

USIRUHUSU MTU AJUE UDHAIFU WAKO.

FIRST DRAFT. 

Maendeleo ni mabadiliko chanya, Maisha ni safari ndefu ambayo inahitaji uvumilivu sana hasa kwa maisha ya kitanzania au Afrika kwa ujumla, vijana wengi wa Tanzania wamekua wakihitaji mafanikio kwa haraka zaidi jambo ambalo kimsingi si sahihi kwa sababu huwezi kufika juu kabla ya kuanza chini ambako lazima ujenge msingi imara utakaokuwezesha kusimama imara, kwa sababu mala nyingi usipojenga msingi mzuri kwa maana ya ( mwanzo au maandalizi) mazuri huwezi kuwa na maisha bora yaliyo endelevu, maisha bora endelevu ni maisha mazuri yasiyo na kikomo.

Kujenga msingi imara ni sifa kubwa ya kujenga maisha mazuri yasiyo na kikomo, watu wengi hufanya mambo pasipokua kujua namna ya kuyafanya kwa sababu wamekosa uelewa wa namna ya kuyafanya mambo hayo. 

Elimu ni muhimu sana kujenga msingi mzuri wa maisha endelevu japo watu wengi wanajua ELIMU NI LAZIMA UKAE DARASANI UFUNDISHWE NA MWALIMU, jambo ambalo kimsingi si sahihi, elimu yoyote uitakayo utaipata ukijituma kusikiliza au kusoma maandiko mbalimbali ya vitabu, majarida, kupitia mtandao / internet. 

Usisikilize maneno ambayo hayajengi (Maneno yenye mtazamo hasi) kutoka kwa watu , mara nyingi watu huwa na maneno yenye mtazamo hasi ambayo kimsingi hurudisha nyuma kama utayatafakari kwa undani zaidi, Kaa na ushinde na watu wenye mitazamo chanya ambayo inauelekeo wa maendeleo. Daima utajifunza mbinu nzuri ambazo zitakusaidia kujenga msingi wa maisha endelevu. 

Panga mipango yako kwa ufasaha na umakini mzuri.

Weka kumbukumbu za mipango yako ya baadaye, Mpango wowote ambao utakujia akilini mwako ni vizuri ukauandikia maandishi na kuyatunza kwa sababu unaweza ukasahau kama unamambo mengi ya kuyashughulikia. Kuweka kumbukumbu husaidia kutumia fursa zozote zitakazojitokeza mbeleyako, kwa maana unaweza ukapata fursa hapo baadaye ukashindwa kuzitumia fursa hizo kwa kuwa na mawazo na Fikra finyu. 
 

Usiruhusu mtu ajue udhaifu wako, kwani kama ni adui yako anaweza kutumia udhaifu wako kukushusha ki-fikra, kwa sababu kushindwa kwa mtu huanzia kwanza katika fikra ndipo kujidhihirisha katika mazingira halisi kwa sababu binadamu hufanya maamuzi kutokana na mambo yaliyomo katika fikra zake. IF YOU THINK SMALL YOU WILL BE SMALL IN YOUR LIFE AND VISE VERSA.

MIPANGO MIZURI YA MAENDELEO HUJA PALE UNAPOKUA KATIKA CHANGAMOTO ZA KIMAENDELEO, KWA HIYO NI VIZURI KUKUMBUKA KUANDIKIA MIPANGO HIYO KABLA HUJAKUTANA NA FURSA.  

mfano mzuri ni huyu jamaa hapa chini anahitaji msaada;
NAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS.
Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo TANZANIA LOANS ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA.
Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusu mikopo ya TANZANIA LOANS pia sikua na uhakika nayo.
Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji.
Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http tanzania-Loans.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs. 95,000 (ELFU TISINI NA TANO) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure!
Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani elfu95 na kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia elfu95 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 3,000,000 (Million 3) hapo nilipo siamini friends.
‪#‎USHAURI‬: Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipanga nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu. Pia kwa yoyote ambae atahitaji kutembelea tovuti ya hawa jamaa wa mikopo, bonyeza hapa: http://tanzania-Loans.wapka.mobiNAHITAJI USHAURI WENU GUYS. BE SERIOUS.
Juzi nilikua napitia Ukurasa wa Vodacom Tanzania nikakuta wameweka Tangazo lao la M-PESA lenye hiyo picha wakihamasisha watanzania wajiunge na Taasisi ya Utoaji mikopo iitwayo TANZANIA LOANS ambayo Vodacom wameingia nao mkataba. Hii Taasisi inatoa mikopo bila RIBA.
Nilisoma tangazo lao na kupuuzia nikawa najua ni matapeli hao wametengeneza page feki ya Vodacom nikaipotezea, sasa jana asubuhi nikakuta tena Tangazo katika ukurasa wa ukweli wa msanii Lady Jaydee nae kapewa dili la kufanya matangazo kuhusu mikopo ya TANZANIA LOANS pia sikua na uhakika nayo.
Usiku wa jana huo huo nikaona sasa Tangazo rasmi katika TV ilikua TBC1 walirusha Live hilo Tangazo katika Taarifa ya Habari za kibiashara wakatoa mpaka website ya Online mtu anaweza kujiunga na akapatiwa mkopo wa pesa na atarudisha mkopo wa pesa bila kua na RIBA halafu marejesho yao mazuri hawambani mkopaji.
Nikasema ngoja nijaribu kujiunga nione je? Niukweli wanatoa mikopo?? Nikafungua website yao jana usiku http tanzania-Loans.wapka.mobi nikasoma maelezo yote! Kuna fomu nikaikuta nikaijaza, nilipoijaza fomu nikapokea ujumbe kua nimefanikiwa kujiunga natakiwa kulipia ada ya Uanachama Tshs. 95,000 (ELFU TISINI NA TANO) ili maombi yangu ya mkopo yaweze kuidhinishwa nipatiwe mkopo. Nikawa naogopa kulipia nisije kutapeliwa bure!
Sasa leo Asubuhi kuna jamaa yangu kumbe nayeye ameshawahi kujiunga na wakampatia kweli mkopo nikamuelezea akanitoa hofu! Nikaona kwani elfu95 na kitu gani?? Ngoja nijaribu nikawatumia elfu95 katika M-PESA wakanitumia ujumbe kua wameipokea pesa nisubirie ndani ya dakika30Nikasubiria, kweli wakanitumia mkopo kupitia M-PESA asubuhi hii ya leo muda si mrefu, niliomba mkopo wa Tshs. 3,000,000 (Million 3) hapo nilipo siamini friends.
#USHAURI: Nifungue mradi gani nina hizi Million Tatu, kwani nilikua sijajipanga nilifanya kama najaribu tu sikua na imani kama ntapata kweli huu mkopo nimejaribu wamenipa! Sijajua biashara ipi ambayo inalipa sana?? Please nisaidieni Mawazo yenu nawaomba! Utani tuweke kando nipo serious katika suala hili nahitaji ushauri wenu. Pia kwa yoyote ambae atahitaji kutembelea tovuti ya hawa jamaa wa mikopo, bonyeza hapa: http://tanzania-Loans.wapka.mobi

MIPANGO MIZURI YA MAENDELEO HUJA PALE UNAPOKUA KATIKA CHANGAMOTO ZA KIMAENDELEO, KWA HIYO NI VIZURI KUKUMBUKA KUANDIKIA MIPANGO HIYO KABLA HUJAKUTANA NA FURSA.
  
Asante sana.
Awadhi Chang'a.
Geographer & Environmentalist.






Friday, August 29, 2014

MTAZAMO CHANYA HUMJENGA MTU KI-FIKRA.

Kuna baadhi ya binadamu ambao huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mawazo na maneno yenye mitazamo hasi ambayo huyapata kutoka kwa wengine, Hii pia ni kawaida tu hasa kwa binadamu yoyote ambaye ambaye ameshapitia misukosuko mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Watu wa namna hii wanahitaji sana mitizamo chanya ambayo Itawajenga ki-fikra,
Kwa sababu wakikumbuka walikotoka na maneno hasi uliyowapa kwaida hujikuta wakiwa wanyonge na walio kata tamaa, Tafadhari fikiri chanya, Ongea mitazamo chanya itakusaidia wewe pamoja na yule unayemueleza. kwa sababu unapoongea mitizamo chanya mala kwa mala, mitizamo hiyo chanya hujiweka katika ufahamu wako na kujikuta unafanya mambo mazuri ya maendeleo.
Ni vizuri sana kufanya, kuongea na kufikiri mitazamo chanya japokua mtazamo chanya hauwezi kujidhihirisha pasipokuwepo na mtizamo hasi kwa maana ili mtizamo chanya ujidhihilishe ni lazima kuwepo na mtizamo hasi kwa hiyo tufanye mitizamo chanya bila kusahau  kuwepo kwa mitazamo hasi ambayo pia ni vizuri kuitambua kusudi kuiepuka na kuikataa ili isikurudishe nyuma kwa maana ya kwamba tuitizame mitazamo hasi pia kwa kuitafutia sululisho la ukweli na uhakika kwa sababu "mtizamo chanya huwezi kuwepo pasipo mtizamo hasi kuwepo". Kwani majukumu ni kuyakabili kwanza.
Na mwisho kabisa kuna mtazamo ambao humuweka mtu katikati "neutral" ambao ni mtazamo ambao mda mwingi haufungamani na upande wowote ule, ambao mala nyingi husaidia kujiepusha na mazara ya kuegamia au kupendelea upande mmoja ambao mala nyingi hutumiwa na viongozi katika kutatua mijadala na mizozo ya makundi mbalimbali ambapo ni VIONGOZI huutumia ili kuleta suruhu. Vilevile ni vizuri kuwatoa watu wenye mitizamo Hasi na kuwapeleka kwenye kundi la watu wenye mitizamo chanya ambao unawajenga, Mbinu Hii  hutumiwa KUSULULISHA MIGOGORO NA MIZOZO MIKUBWA, mfano mzuri wa kiongozi makini ambaye hutumia mbinu hii nzuri ya kutatua Migogoro ni MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ambaye ni Raisi pekee wa Tanzania ambaye anaweza kutatua mizozo ya kisiasa yenye mivutano ya pande mbili, mfano katika hotuba yake ya ufunguzi wa BUNGE LA KUUNDA KATIBA MPYA alijitahidi kuwa kwenye mitizamo ya makundi yote na kutoa faida na hasara za Mitizamo ya makundi hayo na mwisho kabisa akajitahidi kuwavuta wale wenye mitizamo hasi ili wawe kwenye kundi la mtazamo chanya ili wawe wamoja au kitu kimoja na Hii ndo SIFA PEKEE YA MH RAISI J.K aliyonayo ambayo pia ilimfanya awe raisi bora wa Afrika na kupata tuzo ya utawala bora Afrika kwa sababu alishawahi kuwaweka pamoja makundi mawili yaliyokua  yanavutana KENYA ambapo tofauti zao zilisababisha kutokea kwa machafuko nchini mwao. KWA KWELI RAISI J.K ANASTAHILI PONGEZI MAALUM KWANI NI RAISI PEKEE WA TANZANIA ANAYEKUZA DEMOKRASIA, UELEWA (Elimu) NA UHURU, UKWELI KWA WANANCHI.
Mtizamo huu ni mzuri lakini ni vizuri kujitahidi kuegemea kwenye mtizamo chanya kwa sababu hauna madhara malanyingi HUMJENGA MTU NA KUMUEPUSHA NA MISUKOSUKO.
Mtazamo Chanya humjenga mtu kwa sababu mambo unayoyafikiri siku zote ndo zao kuu la maisha yako ya baadae kwa hiyo kama Unamtazamo chanya kwa kufikiria na kufanya mambo yako baasi jihesabie ya kwamba ni mtu mwenye maisha mazuri siku za usoni au za hapo baadaye, vile vile mambo yote unayoyafikilia huwa ndo muelekeo wako wa baadaye "IF YOU THINK SMALL YOU WILL BE SMALL ON YOUR LIFE".  
Hebu angalia mfano huu mdogo wa A Lincolin ambaye kimtazamo alitaka kurudishwa nyuma lakini hakukubaliana na hari kama hiyo kwa hiyo USIKUBALI KURUDISHWA NYUMA KWA MANENO MATUPU TU, Kwani wengine hujiona WAMESHINDWA kwa sababu ya maneno hasi ya watu, na kujikuta Wanafikiria kushindwa, ambapo fikra hizo hujengeka nafsini / akilini mwao na kujikuta wameshindwa kwa sababu fikra hizo zimejengeka akilini na nafsini mwao. SI VIBAYA KAMA UTAKUA UNAFIKIRI MITIZAMO CHANYA KWA SABABU ITAKUJENGA. Lakini si vibaya sana kama utajifunza kuitetea mitazamo yako CHANYA popote pale na kwa mtu yoyote. kwa maana mitizamo chanya huanza kujidhihirisha kutoka kwenye fikra hadi kwenye utekelezaji na utendaji wako.



"ALWAYS THINK POSITIVE TO RECEIVE POSITIVITY"
"UNAPOTEMBEA ANGALIA MBELE USITEMBEE UKIANGALIA NYUMA UTAANGUKA" 
Thanks
Awadhi Chang'a
Geographer & Enviromentalist


Thursday, August 28, 2014

JIFUNZE KUTUMIA FURSA ULIZO NAZO sehemu ya 1.

UBUNIFU ni sifa kubwa sana za kukuwezesha mradi wako uendelee vizuri na kupata mafanikio kwa maana ili uweze kufanikisha mradi wako ni lazima uwe na jambo jipya ambalo watu watalipokea kwa muamko mkubwa kwa maana mambo mapya hupendwa zaid au huwa na soko kubwa sana.
Wajasiliamali/Wafanyabiashara wanashauliwa kuwa wabunifu kwa maana watapata masoko kwa bidhaa zao kwa sababu utakua peke yako kwa hiyo utapata wateja wengi sana tofauti na kufanya biashara ambazo kila mtu anazifanya katika eneo lako kwa hiyo itapunguza ushindani katika biashara na kukupa fursa wewe za kufanikiwa, kwa mfano ukifungua duka la nafaka sehemu ambayo kuna maduka ya nafaka ni kokosekana kwa UBUNIFU katika kazi zako kwa hiyo hutaendelea mbele zaid.
Ubunifu unaweza kuupata wapi? au mambo yanayoweza kukusaidia kuwa mbunifu?, Kujifunza nchi za Nje au jirani wanafanya nini kwa wakati huu Mfano KUTEMBELEA NCHI ZA JIRANI, Ukweli wa mambo ni kwamba mambo mengi hutoka nchi za jirani na kuja kwetu Tanzania, kwa hiyo kilichofika Tanzania BASI NCHI ZA WENZETU KIMECHAKAA, Ni mambo machache ambayo huanzia hapa kwetu, asilimia kubwa yanatoka nje kwa hiyo jifunze ni nini wanafanya nchi za wenzetu afu unaweza ukapata ujuzi na kukuza maalifa juu ya kitu hicho na kukifanyia kazi.
VILE VILE kuboresha UBUNIFU wa mwenzio pia ni mbinu mojawapo ya kukuwezesha kutoka na kitu kipya ambacho kitakubaliwa na wakazi wote.
Kufanya TAFITI itasaidia sana kutoka na kitu kipya ambacho kitaleta manufaa kwako  na mwisho kabisa ni KUJIELIMISHA kwa kusoma majarida, magazeti, kutumia mtandao/ internet, taarifa mbalimbali.
Kwa mfano mzuri kabisa, Fursa zilizopo sasa zinatoka kwenye Umoja wa Afrika Mashariki ambao kwa sasa wanalengo la kukuza mahusiano ya kiuchumi, kisiasa na kijamiii ambao wana muelekeo wa kuja kuwa kama taifa moja lililo ungana kiuchumi, kisiasa na kijammii. kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutafuta UBUNIFU kutoka kwa majirani zetu ili kujiendeleza kiuchumi, milango ipo wazi sasa na kazi ni kwako KUTUMIA FURSA.

Asante;
Awadhi Chang'a
Geographer.


Wednesday, August 27, 2014

NENO NI SILAHA.

TUJIFUNZE KUFANYA TAFITI, KUSOMA NA KUELEWA MAMBO NDIPO TUTOE KAULI NA KUONGEA MAMBO... USISIKIE TU JAMBO NA KUKURUPUKA KULITOA NA KULISAMBAZA KWANI MANENO NI SILAHA AMBAYO INAWEZA KUALIBU AU KUTENGENEZA JAMBO VILE VILE NENO LINAWEZA KUMUALIBU MTU AU KUMPA AHUENI MTU... KWA HIYO USITHUBUTU KUONGEA JAMBO BILA KUFANYA UTAFITI, UKISHINDWA WAACHE WENGINE WALIFANYIE HITIMISHO NA KULITOLEA MAAMUZI.
Awadhi Chang'a - Geographer

Saturday, March 22, 2014

HOTUBA YA MH RAISI DR JK YAZUA MJADARA

 
Watanzania wavivu sana kuchambua mambo au Hawasikilizi kitu vizuri au hawasikilizi kuanzia mwanzo hadi mwisho au inawezekana wangi wenu mlichelewa kuisikiliza hotuba kwa hiyo mmesikia baadhi ya sehemu na wengine wanasema ili waonekane wamechangia jambo na mwisho kabisa wengine ni washabiki wa vyama vya kisiasa bila kusahau wengine hawampendi raisi wao na kumtakia mema... hapana simaanishi wewe aaaah ni wengine tu... mheshimiwa DR jakaya Mrisho Kikwete amegusia mambo yote hajazungumzia jambo moja amechambua kila jambo kwa kutoa faida na hasara za kila jambo... sasa kwa kuwa wabongo wanajua kukuza mambo bhaas hawajaangalia ubora wa ile hotub kwa ujumla... usisahau kila kizuri kina kasolo.... YEYE AMEWAACHIA KAZI WAJUMBE WA BUNGE LA KATIBA KWA KUWAHUSIA WAJUMBE MAMBO MENGI LICHA YA TOFAUTI ZAO ZA KIDINI, KISIASA, WATENGENEZE KATIBA ITAKAYO STAWISHA DEMOKRASIA MAENDELEO, UMOJA N.K... PIA ALISISITIZA KWAMBA KILA MJUMBE AWE NA MSIMAMO WAKE NA ASISIKILIZE NA KUAMULIWA NA MTU... KWA HIYO MHESHIMIWA RAISI DR JK AMEWAPA UHURU WA KUJIAMULIA MAMBO YAO WENYEWE HATA KAMA NI SERIKALI TATU... NA MWISHO ALITOA MSIMAMO WAKE WA MFUO WA SERIKALI MBILI KWA KUTOA ATHARI YA KUZALIWA TAIFA JINGINE LA TANGANYIKA... kwa hiyo kwa mantiki hiyo kutakua na serikali ya tanganyika inayomiliki lasilimali zake, serikal ya zanzibar inayomiliki lasilimali zake na serikali ya tatu ni serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ambayo kimsingi inategemea mchango kutoka serikali ya tanganyika na zanzibar... sasa ikitokea serikali hizo mbili zikgoma kuchangia uendeshaj wa serikali wa jamuhuli nini kitachotokea... ina maanisha serikali ya jamuhur ambayo inamiliki vyombi vya ulinzi na usalama itashindwa kuwalipa madai yao na kusababisha ugomvi na mapinduzi ya jeshi na vita ya wajesh na wananchi pia Mh DR JK aliendelea kwa kutoa mifano ya migogoro mbali mbali ya kisiasa ya nchi nyingi ambayo imesababishwa na mifumo kama hii ambayo wananchi wanataka iwe mfano taifa kubwa kama urusi pia lilibomolewa kwa namna hii hii kwa sababu raisi wa serikali ya jamuhuli ya muungano anakosa nguvu kwa muundo huu... vile vile bada ya kufa kwa muungano watanzania walioungana kidamu mtawaambia nn eti wewe sio mzanzibar basi ondoka hapa kahame uende kwenu wee MENGI YALIONGELEWA...KWA KWELI ANASTAHIRI PONGEZI KWA HOTUBA NZURI AMBAYO AMETUMIA MDA WAKE KUANDAA KWA AJIRI YA UFUNGUZ WA BUNGE MAALUM. AFU ALIKUWA MFANISI SANA KWANI HAJASOMA AMEITOA KICHWANI MWAKE NA KWA HILO ANAKAMILISHA USEMI ULE USEMAO YEYE NI DAKTARI ALIYE BOBEA KATIKA KUTATUA MIZOZO YA KISIASA...

Sunday, January 19, 2014

ARSENAL IN THE FIRST PLACE

Chelsea's Oscar
Chelsea's Oscar (C) is challenged by Manchester United's Michael Carrick (R) during their English Premier League soccer match at Stamford Bridge in London, January 19, 2014. (Photo : Reuters) "

The English Premier League table has Arsenal in first place and they lead Manchester City and Chelsea in the EPL standings heading into play on Monday and after the results on Sunday and it comes as the Blues defeated Manchester United at Stamford Bridge and they got three goals in the match from Samuel Eto'o and now they are in good position heading into next week in the EPL standings.

Sunday play saw Chelsea win 3-1 over Man U and it was a tough loss for Manchester at Stamford Bridge and that came after the early match saw Swansea City lose at home against Tottenham Hotspur after two goals from Emmanuel Adebayor. The Table is tight at the top and now the Gunners are in first place after winning on Saturday and they are up on top of Manchester City and Chelsea remains in third place after their positive result and Liverpool is in fourth position ahead of Everton and Tottenham played well on Sunday and now they are in sixth place ahead of Manchester United and Man U stays in position now in seventh and they are ahead of Newcastle and Southampton.

Like Us on Facebook

The matches on Saturday started up with a draw between Sunderland and Southampton after goals from Adam Johnson and Jay Rodriguez and then Arsenal took Fulham 2-0 to stay on top of the league table with two goals from Santi Cazorla in the second half. The Gunners have been playing very well and they remain in first place in the Barclays EPL and the other matches on the day includes Crystal Palace getting a win against Stoke City at home and Manchester City played very well at the Etihad and they won 4-2 against Cardiff and they got goals from Yaya Toure and Jesus Navas.

Norwich City won over Hull and West Ham United lost to Newcastle after two goals from Yohan Cabaye and in the late game on Saturday, Liverpool pulled even with Aston Villa at the Anfield with goals from Daniel Sturridge and Steven Gerrard. Monday finishes the week schedule with west Brom and Everton playing and then on Tuesday next week things pick up with a full schedule of Manchester United, Norwich, Arsenal, Liverpool and Everton all in action and then on Wednesday there is Manchester City and Tottenham in the late match with Chelsea also in action.

Check here for the ESPN results and table for the English Premier League.