Ngazi ni kifaa ambacho hutumika kuzifikia sehemu za juu ambazo hazifikiki kiurahisi. Sehemu za juu aidha huwa na kitu muhimu sana kwa wakati huo au Mda wote.
Binadamu wa kileo hutumia sana Ngazi, Lakini si ngazi hizo tunazo zifahamu kufikia mafanikio ambapo dhuluma, ukandamizaji, unyang'anyi, udanganyifu na mengine mengi sana mabaya ambayo Binadamu huyafanya Ili kujiingizia kipato kiurahisi pasipo kufanya jitihada zozote.
Inasikitisha sana kuona mataperi wanazidi kuongezeka siku hadi siku, watu wanakaa wanajadili namna ya kuingiza kipato pasipo kuvuja jasho.
Magufuli amefanya juhudi kubwa ya kutengeneza Tanzania mpya lakini bado wasio na taaluma au uelewa wanaliwa pesa pasipo kujua wanaliwa.
Usipo kuwa makini ukajikuta unatoa fedha pasipo kuwa na haja ya kutoa pesa. Matapeli wanakaa wanajadili namna ya kuingiza kipato pasipo kufanya jitihada zozote. je ? unapenda kutapeliwa. Kama jibu ni Hapana Bhaaasi endelea kufuatilia nakala hii