SAIDIA JAMII, JAMII ITAKUSAIDIA.
Mchakato wa kuleta mabadiliko katika jamii husaidia wataalamu kuzifikia ndoto zao za maisha bora kwa sababu jamii hiyo unayoisaidia automatically will pay you back kwa maana jamii inahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wataalam mbalimbali, kwa sababu kuna matatizo mbalimbali yanayotuzunguka ambayo hayajapatiwa suruhisho hadi sasa. je huamini kama jamii itakupa manufaa kwa kuisaidia anza sasa na utaona mabadiliko makubwa sana katika maisha yako.
Huu ni mchakato maalum kwa ajili ya kuwaelimisha wataalama ili waweze kusaidia jamii zao zinazowazunguka, kwa maana hadi sasa mambo mengi ya kusaidia jamii na mazingira yanayowazunguka yanafanywa na mashirika ya kigeni ya wazungu, wachina n.k... kwa mfano WCS, WWF ni mashirika ambayo makao makuu yako nchi za nje, Hii inadhihirisha dhahiri kwamba tumetawaliwa hadi kifikra na mtazamo kwa sababu tumeziacha fikra zetu zilale na kusababisha wageni kuja kutufanyia mambo ya kusaidia jamii na mali asili zetu ili zisipotee, ni jambo la kusikitisha sana kuona sisi wenyewe hatuoni umuhimu wa kuwa pamoja ili kuipigania nchi yetu na kutunza mali asili zetu na kuijenga nchi yetu kwa manufaa yetu wenyewe, ivi unadhani huyo mgeni atafanya hizo kazi kwa uchungu bila kuiba rasilimali zetu. amka wewe mtaalam wa kitanzania jengeka kifikra acha kubaki na vitu vizuri katika kichwa bila kuvitoa kwa jamii ili visaidie kujenga jamii yetu ili tusiendelee kuwategemea wageni. wageni hawa hawawezi kuwa na uzalendo asilimia mia 100%.
Angalia leo dola ya Mmarekani inavonyanyasa shilingi ya kitanzania Ambapo dola moja 1 ni sawa na shilingi elfu mbili 2,000. Acha kulalamika umaskini wakati wewe mwenyewe ndo unayeikubali hali hii ya maisha kwa maana kufanya kazi kwa bidii ndo zao la maisha bora jitume kusaidia jamii, kujenga fikra zako mwenyewe na za wengine.
Wasomi au wataalam waliowengi walitegemeamambo makubwa sana siku zao za usoni hasa pale wanapo anza kupata taaluma zao na baada ya kuanza kufanya kazi zao zinazowaingizia kipato. Mtazamo huu ni mzuri sana lakini kuna changamoto nyingi sana ambazo huwakabili wataalam walio wengi na kujikuta wamekata tamaa kuzikamilisha ndoto zao za maisha bora. Hii husababishwa na wataalam kuto kujua maslai ya kuisaidia jamii, hakuna jambo lolote linalolipa hapa duniani kama kusaidia jamii na mazingira yake. Lazima tujue kusaidia jamii ndo kipaombele cha taaluma zetu tunazopewa mashuleni na walimu Kwa hiyo baasi taaluma ni msingi wa kuleta mabadiliko na kutatua changamoto za maisha ya jamii na mazingira yake. lakini wataalam au wasomi walio wengi wanakabiliwa na tatizo la kulala kwa fikra ambazo ni za muhimu sana katika taifa letu. tafadhari amsha fikra zako acha kulaza fikra zako ni hasara kubwa sana kwa taifa letu.
Wataalam wanafikra nzuri na wanafahamu mbinu za kujiimarisha kifikra lakini fikra zao mala nyingi hulala kwa sababu ya mambo mengi ya kiteknolojia. Waliowengi wanajikuta addicted kwa baadhi ya vitu vya kisasa ambavyo kimsingi havimsaidii kumjenga kifikra na mitazamo ya kuiendeleza taaluma yake ili aisaidie jamii kwa mfano kuwa addicted na matumizi ya social media.
Jambo lingine wataalam waliowengi wanavipa vipaombele vitu ambavyo ambavyo haviimarishi taaluma zao na fikra zao. Katika mijadara yao ya kila siku hujikuta wakijadili mambo ya burudani kwa mfano Dimond Platnum anatoka na nani. Mijadala isiyo na mantiki husaidia katika kudumaza taaluma zao kwa maana mala nyingi mijadala husaidia kuamsha fikra zilizo lala kwa maana ili jambo liwe kwenye utekelezaji wa mtu binafsi linahitaji kukumbushwa mala kwa mala ili akili ipate kuliona umuhimu wa jambo hilo.Vile vile wataalam hao hao katika mijadala ya makundi mbalimbali ya jamii wao ndo wamekua mstali wa mbele kuongoza ama kusapoti mijadala isiyo na tija, hatukatai kuongelea mambo pendwa lakini yasiwe ndo msingi wa mazungumzo yenu kwa sababu yatadumaza fikra za maendeleo. Tusipokua makini tutaendelea kumtegemea mzungu katika kutuendeshea mambo yetu na sisi tutabaki tukipiga polojo tu zisizo na maana. TAFADHARI USIPIGE POLOJO TOA FIKRA JENZI.
KUWA MZALENDO SAIDIA JAMII JAMII ITAKUSAIDIA
ITAENDELEA TOLEO LIJALO
yafuatayo yatakuwemo
1. namna ya kujijenga kifikra
2. namna ya kutumia taaluma yako kuisaidia jamii
3. ni kwa namna gani utapata manufaa kwa kuisaidia jamii, na mengine mengi
TAFADHARI UNAOMBWA KUCHANGIA ILI KUENDELEZA UFANISI WA BLOGU HII KWA MAANA MCHANGO WAKO UNASAIDIA SANA KATIKA KUHAKIKISHA ZOEZI LA UTAFITI ILI KUTOA ELIMU KWA KINA NA KWA UKAMILIFU. TAFADHARI UNAOMBWA KUCHANGIA KUPITIA NAMBA YA M-PESA 0752393944.
CHANGIA ILI KUKUZA UFANISI WA BLOG HII MCHANGO WAKO NDO NGUZO NA MSINGI WA KUPEANA UFANISI CHANGIA SASA.
NB: NAKALA HII BADO IPO KWENYE MABORESHO
Awadhi Chang'a.
Geographer & Environmentalist.
awadhchang@outlook.com
0752-393944.