Friday, August 29, 2014

MTAZAMO CHANYA HUMJENGA MTU KI-FIKRA.

Kuna baadhi ya binadamu ambao huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mawazo na maneno yenye mitazamo hasi ambayo huyapata kutoka kwa wengine, Hii pia ni kawaida tu hasa kwa binadamu yoyote ambaye ambaye ameshapitia misukosuko mbalimbali katika maisha yake ya kila siku. Watu wa namna hii wanahitaji sana mitizamo chanya ambayo Itawajenga ki-fikra,
Kwa sababu wakikumbuka walikotoka na maneno hasi uliyowapa kwaida hujikuta wakiwa wanyonge na walio kata tamaa, Tafadhari fikiri chanya, Ongea mitazamo chanya itakusaidia wewe pamoja na yule unayemueleza. kwa sababu unapoongea mitizamo chanya mala kwa mala, mitizamo hiyo chanya hujiweka katika ufahamu wako na kujikuta unafanya mambo mazuri ya maendeleo.
Ni vizuri sana kufanya, kuongea na kufikiri mitazamo chanya japokua mtazamo chanya hauwezi kujidhihirisha pasipokuwepo na mtizamo hasi kwa maana ili mtizamo chanya ujidhihilishe ni lazima kuwepo na mtizamo hasi kwa hiyo tufanye mitizamo chanya bila kusahau  kuwepo kwa mitazamo hasi ambayo pia ni vizuri kuitambua kusudi kuiepuka na kuikataa ili isikurudishe nyuma kwa maana ya kwamba tuitizame mitazamo hasi pia kwa kuitafutia sululisho la ukweli na uhakika kwa sababu "mtizamo chanya huwezi kuwepo pasipo mtizamo hasi kuwepo". Kwani majukumu ni kuyakabili kwanza.
Na mwisho kabisa kuna mtazamo ambao humuweka mtu katikati "neutral" ambao ni mtazamo ambao mda mwingi haufungamani na upande wowote ule, ambao mala nyingi husaidia kujiepusha na mazara ya kuegamia au kupendelea upande mmoja ambao mala nyingi hutumiwa na viongozi katika kutatua mijadala na mizozo ya makundi mbalimbali ambapo ni VIONGOZI huutumia ili kuleta suruhu. Vilevile ni vizuri kuwatoa watu wenye mitizamo Hasi na kuwapeleka kwenye kundi la watu wenye mitizamo chanya ambao unawajenga, Mbinu Hii  hutumiwa KUSULULISHA MIGOGORO NA MIZOZO MIKUBWA, mfano mzuri wa kiongozi makini ambaye hutumia mbinu hii nzuri ya kutatua Migogoro ni MH. JAKAYA MRISHO KIKWETE ambaye ni Raisi pekee wa Tanzania ambaye anaweza kutatua mizozo ya kisiasa yenye mivutano ya pande mbili, mfano katika hotuba yake ya ufunguzi wa BUNGE LA KUUNDA KATIBA MPYA alijitahidi kuwa kwenye mitizamo ya makundi yote na kutoa faida na hasara za Mitizamo ya makundi hayo na mwisho kabisa akajitahidi kuwavuta wale wenye mitizamo hasi ili wawe kwenye kundi la mtazamo chanya ili wawe wamoja au kitu kimoja na Hii ndo SIFA PEKEE YA MH RAISI J.K aliyonayo ambayo pia ilimfanya awe raisi bora wa Afrika na kupata tuzo ya utawala bora Afrika kwa sababu alishawahi kuwaweka pamoja makundi mawili yaliyokua  yanavutana KENYA ambapo tofauti zao zilisababisha kutokea kwa machafuko nchini mwao. KWA KWELI RAISI J.K ANASTAHILI PONGEZI MAALUM KWANI NI RAISI PEKEE WA TANZANIA ANAYEKUZA DEMOKRASIA, UELEWA (Elimu) NA UHURU, UKWELI KWA WANANCHI.
Mtizamo huu ni mzuri lakini ni vizuri kujitahidi kuegemea kwenye mtizamo chanya kwa sababu hauna madhara malanyingi HUMJENGA MTU NA KUMUEPUSHA NA MISUKOSUKO.
Mtazamo Chanya humjenga mtu kwa sababu mambo unayoyafikiri siku zote ndo zao kuu la maisha yako ya baadae kwa hiyo kama Unamtazamo chanya kwa kufikiria na kufanya mambo yako baasi jihesabie ya kwamba ni mtu mwenye maisha mazuri siku za usoni au za hapo baadaye, vile vile mambo yote unayoyafikilia huwa ndo muelekeo wako wa baadaye "IF YOU THINK SMALL YOU WILL BE SMALL ON YOUR LIFE".  
Hebu angalia mfano huu mdogo wa A Lincolin ambaye kimtazamo alitaka kurudishwa nyuma lakini hakukubaliana na hari kama hiyo kwa hiyo USIKUBALI KURUDISHWA NYUMA KWA MANENO MATUPU TU, Kwani wengine hujiona WAMESHINDWA kwa sababu ya maneno hasi ya watu, na kujikuta Wanafikiria kushindwa, ambapo fikra hizo hujengeka nafsini / akilini mwao na kujikuta wameshindwa kwa sababu fikra hizo zimejengeka akilini na nafsini mwao. SI VIBAYA KAMA UTAKUA UNAFIKIRI MITIZAMO CHANYA KWA SABABU ITAKUJENGA. Lakini si vibaya sana kama utajifunza kuitetea mitazamo yako CHANYA popote pale na kwa mtu yoyote. kwa maana mitizamo chanya huanza kujidhihirisha kutoka kwenye fikra hadi kwenye utekelezaji na utendaji wako.



"ALWAYS THINK POSITIVE TO RECEIVE POSITIVITY"
"UNAPOTEMBEA ANGALIA MBELE USITEMBEE UKIANGALIA NYUMA UTAANGUKA" 
Thanks
Awadhi Chang'a
Geographer & Enviromentalist


Thursday, August 28, 2014

JIFUNZE KUTUMIA FURSA ULIZO NAZO sehemu ya 1.

UBUNIFU ni sifa kubwa sana za kukuwezesha mradi wako uendelee vizuri na kupata mafanikio kwa maana ili uweze kufanikisha mradi wako ni lazima uwe na jambo jipya ambalo watu watalipokea kwa muamko mkubwa kwa maana mambo mapya hupendwa zaid au huwa na soko kubwa sana.
Wajasiliamali/Wafanyabiashara wanashauliwa kuwa wabunifu kwa maana watapata masoko kwa bidhaa zao kwa sababu utakua peke yako kwa hiyo utapata wateja wengi sana tofauti na kufanya biashara ambazo kila mtu anazifanya katika eneo lako kwa hiyo itapunguza ushindani katika biashara na kukupa fursa wewe za kufanikiwa, kwa mfano ukifungua duka la nafaka sehemu ambayo kuna maduka ya nafaka ni kokosekana kwa UBUNIFU katika kazi zako kwa hiyo hutaendelea mbele zaid.
Ubunifu unaweza kuupata wapi? au mambo yanayoweza kukusaidia kuwa mbunifu?, Kujifunza nchi za Nje au jirani wanafanya nini kwa wakati huu Mfano KUTEMBELEA NCHI ZA JIRANI, Ukweli wa mambo ni kwamba mambo mengi hutoka nchi za jirani na kuja kwetu Tanzania, kwa hiyo kilichofika Tanzania BASI NCHI ZA WENZETU KIMECHAKAA, Ni mambo machache ambayo huanzia hapa kwetu, asilimia kubwa yanatoka nje kwa hiyo jifunze ni nini wanafanya nchi za wenzetu afu unaweza ukapata ujuzi na kukuza maalifa juu ya kitu hicho na kukifanyia kazi.
VILE VILE kuboresha UBUNIFU wa mwenzio pia ni mbinu mojawapo ya kukuwezesha kutoka na kitu kipya ambacho kitakubaliwa na wakazi wote.
Kufanya TAFITI itasaidia sana kutoka na kitu kipya ambacho kitaleta manufaa kwako  na mwisho kabisa ni KUJIELIMISHA kwa kusoma majarida, magazeti, kutumia mtandao/ internet, taarifa mbalimbali.
Kwa mfano mzuri kabisa, Fursa zilizopo sasa zinatoka kwenye Umoja wa Afrika Mashariki ambao kwa sasa wanalengo la kukuza mahusiano ya kiuchumi, kisiasa na kijamiii ambao wana muelekeo wa kuja kuwa kama taifa moja lililo ungana kiuchumi, kisiasa na kijammii. kwa hiyo watanzania wanatakiwa kutafuta UBUNIFU kutoka kwa majirani zetu ili kujiendeleza kiuchumi, milango ipo wazi sasa na kazi ni kwako KUTUMIA FURSA.

Asante;
Awadhi Chang'a
Geographer.


Wednesday, August 27, 2014

NENO NI SILAHA.

TUJIFUNZE KUFANYA TAFITI, KUSOMA NA KUELEWA MAMBO NDIPO TUTOE KAULI NA KUONGEA MAMBO... USISIKIE TU JAMBO NA KUKURUPUKA KULITOA NA KULISAMBAZA KWANI MANENO NI SILAHA AMBAYO INAWEZA KUALIBU AU KUTENGENEZA JAMBO VILE VILE NENO LINAWEZA KUMUALIBU MTU AU KUMPA AHUENI MTU... KWA HIYO USITHUBUTU KUONGEA JAMBO BILA KUFANYA UTAFITI, UKISHINDWA WAACHE WENGINE WALIFANYIE HITIMISHO NA KULITOLEA MAAMUZI.
Awadhi Chang'a - Geographer